Tanzania emblem

Tanzania Fertilizer Regulatory Authority

Announcements

TAARIFA KWA UMMA: TFRA INATOA SIKU 45 KWA WAFANYABIASHARA KUSAJILI MBOLEA ZOTE ZISIZOSAJILIWA


Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA) inapenda kuwataarifu watengenezaji, wazalishaji, waingizaji, wasambazaji na wafanyabiashara wote wa mbolea hapa nchini kuwa kwa mujibu wa Sheria ya Mbolea Namba 9 ya Mwaka 2009 kifungu 8 (1), mbolea zote, yabisi na maji (foliar fertilizers) zinazozalishwa au zinazoingizwa na kuuzwa hapa nchini lazima ziwe zimesajiliwa na kupewa kibali na Mamlaka ya udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA).

Hivyo, kwa kuzingatia matakwa ya kisheria, Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania inatoa muda wa siku 45 kuanzia tarehe 11/01/2021 hadi tarehe 24/02/2021 kwa watengenezaji, wazalishaji, waingizaji, wasambazaji na wafanyabiashara wote wa mbolea kuhakikisha kuwa mbolea zote wanazozitengeneza au kuziingiza na kuziuza hapa nchini zimesajiliwa na TFRA. Kuanzia 25 /02/2021 Mfanyabiashara yeyote atakayekutwa na mbolea ambayo haijasajiliwa atachukuliwa hatua kali za kisheria.

Kwa mujibu wa Sheria ya Mbolea, Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA) ina jukumu la kudhibiti ubora wa mbolea zote zinazotengenezwa au zinazoingizwa hapa nchini na kusambazwa kwa wakulima.

Imetolewa na

Dkt. Stephan E. Ngailo

MKURUGENZI MTENDAJI

11 Januari 2021